Wednesday, December 10, 2014

VCCT Siku tatu za matumaini na Johannes Amritzer

KONGAMANO LA "SIKU TATU ZA MATUMAINI"

MAHALI: VICTORY CHRISTIAN CENTRE TABERNACLE, MBEZI BEACH A, KUSHOTO BAADA YA DARAJA LA MTO MBEZI, BARABARA YA MWAI KIBAKI)

RATIBA RATIBA:
IJUMAA, 12 DEC 2014: SAA 11-12:30JIONI.
JUMAMOSI, 13 DEC 2014: SAA 9 ALASIRI -12:30JIONI.
JUMAPILI, 14 DEC 2014:
IBADA YA KWANZA(ENGLISH): SAA 1-3:30ASBH
IBADA YA PILI(SWAHILI): SAA 4-6:30MCHN.
KIPINDI CHA JIONI: SAA 9:30-12:30 JIONI

USAFIRI KUTOKA NA KURUDI MAKUMBUSHO, MWENGE NA TEGETA UTAKUWEPO NUSU SAA (DAKIKA 30) KABLA YA KILA KIPINDI. USICHELEWE.

KILA MTU DAR ES SALAAM ATAHUDHURIA, USIKOSE NAWE PIA

MAWASILIANO:
SIMU: 0762 441 719, 0714 503 638
EMAIL: info@vcc.or.tz, WEBSITE: www.vcc.or.tz
FACEBOOK: https://www.facebook.com/pages/Victory-Christian-Centre-VCC/222284597835014
BLOG: http://vcctcampusministry.blogspot.com/



Tuesday, December 2, 2014

Papaa On Tuesday.....Hisia/Mihemko ya Nafsi huzuia Upeo Wa Kufikiri Sawasawa.

Mimi na wewe tunayo sababu ya Kumshukuru Mungu kutupa fursa ya kuweza kuona mwezi wa mwisho kabisa kuweza kumaliza mwaka 2015.

Wiki jana taifa lilikuwa limezizima kwa sababu ya issue ya Bungeni kuhusiana na Escrow. Wabunge walitekwa na hisia kali wakati wa kuchangia wengine kutokana na mapenzi yao makubwa na itikadi zao wakajikuta wanahamaki na kupoteza uwezo wa kuchambua mambo.

Hisia za kiitikadi, imani za dini, mapenzi, furaha ama huzuni ni baadhi ya vitu vinavyopofusha uwezo wa kufikiri katika maisha. Si vibaya kuwa na hisia kwenye jambo fulani ila hisia kali hupofusha uwezo wa kupambanua mambo.

Unapokuwa na mapenzi mazito na chama cha siasa ama shabiki wa timu ya mpira wa miguu na ukaruhusu hisia zako zitawale uwezo wako wa ku analyze mambo basi wengi wetu hujikuta yale tunayoyaongea yakatugharimu siku tukiwa katika hali ya kawaida. Bungeni nilisikia watu wazima wakiongea "kisiasa" zaidi kuliko uhalisia wa mambo mwisho wa hisia ni majuto.

Kuna maamuzi tumewahi kayachukua tukiwa katika lindi la mapenzi ambayo kwa sasa yanatugharimu. Kuna wengine wamejikuta kwa sasa wana vilema vya kwenye maisha kutokana na mapenzi, kuna watu wamejikuta wamekuwa na watoto si kwa sababu walipanga la hasha sababu wakati wa maamuzi walikuwa kwenye wimbi la mapenzi. Wapo ambao walipokuwa kwenye mapenzi walionywa na ndugu zao na jamaa zao lakini hawakusikiliza wakajikuta wanapata mimba na baadae kuzitoa matokeo yake mpaka leo kutendo hicho kinawahukumu. Mengi ya maamuzi haya yalifanyika tukiwa katika lindi la mapenzi na tuliona tunafanya sahihi na tukasahau kuwa hisia zetu kali zina athiri uwezo wetu wa kupambanua mambo.

Miaka michache iliyopita waliibuka watu waliokuwa na imani watapanda ndege na kwenda nje ya nchi pasipo kuwa na ticket ya ndege wala Visa. Huu uwezo wa imani kiasi hiki huathiri sana uwezo wa kupambanua mambo. Hisia za kidini zimesababisha mara nyingi mihemko ya maamuzi ya kupelekea wengine kuwa na uwezo wa kujitoa uhai a.k.a kujitoa muhanga. Watu hawapendi kuhojiwa katika kile wanachokiamini kwa sababu tu ni dhehebu lao. Ukiwauliza kwanini mnabatiza kwa maji mengi?badala ya kujibu hoja watu wanakuwa wakali. Hivi tunaishi katika kizazi gani ambacho udadisi unaogopwa?. Miaka michache iliyopita nchini Uganda tulishuhudia baadhi ya waumini wakichomwa moto si kwamba watu walikuwa hawajui la hasha walitekwa na hisia za dini ya Kibwetere.

Nyakati ambazo tunahisia kali za furaha mara nyingi tulijikuta tukitoa ahadi ambazo tukiwa na akili timamu tuliishia kutubu na kujuta. Furaha zetu zilitufanya tuone tunaweza kutenda, furaha zetu pengine zilisababisha tukatoa na fedha ambazo tungekuwa normal tusingediriki kutoa kiasi hicho cha pesa. Wengine kwa sababu ya hisia za kusifiwa pengine kutokana na ulivyo ama ulivyotenda ulijikuta umelewa sifa na kusababisha utende matendo ambayo ulipokywa na akili timamu ulibaki kujishangaa uliwezaje kufanya jambo hilo. Pengine watu walikusifia kwa ulichokifanya ila watu hawajui kuwa muda huo moyo wako na akili zako zilikiwa Zimepotoshwa na furaha.

Si furaha tu wengine ni hasira, wengine wakiwa na hasira wanatupa vitu hovyo, wengine huamua ku delete baadhi ya watu, wengine kwa kushindwa ku control hisia zao hujikuta wameongea mambo ambayo badala ya kutatua tatizo wanaleta tatizo lingine. Kuwa mwangalifu nini unafanya na kuongea unapokuwa ume kasirika maneno unayoyaongea yanaweza kusababisha ukaeleweka vibaya hata kama ulikuwa na nia nzuri. Misongo ya mawazo na machungu ya moyoni hulipuka kama volkano hai katikati ya miamba. Migogoro mingi inapokwisha hata kwenye ndoa na mkasameheana kupona ama kubaki na jeraha inategemeana sana na yale uliyoyaongea wakati ume loose control ya ubongo. Unakuta mtu anafunguka "mie mwenyewe nakuvumilia mume wangu we huwaoni wanaume wenzio kama akina Robert, Kweka wanavyochakalika wale ndo wanaume".....haya maneno hata kama ugomvi utaisha yataendelea kusikika kwenye moyo wa mwanaume. Hasira hasara unaweza ukawa unaongea jambo la maana sana ila HISIA zako zikakusabisha usione Ubaya wa kile kinachosema. Fikiri kabla yq kutenda.

Kama kuna siku ulijibishana na mtu kwenye sms ama kwenye mitandao hasira zikiisha kasome yale uliyoandika ndipo utajua hisia zenye hasira husababisha majanga makubwa sana maishani. Jifunze kujirudi pale unapoona mambo yamekuwa sio mambo, sifa za kijinga hazitakusaidia.

Kumbuka Hisia hupofusha akili katika maamuzi.

Think Differently and Make a difference.

Ze Blogger.
0713 494110